Skip to main content

Maamuzi muhimu katika kuikabili kesho yako.

 Somo hili lilifundishwa na Juvenalis Makatu ambaye ni Raisi wa serikali ya wanafunzi chuo cha afya Musoma.

Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/maamuzi

Maamuzi ni azimio linalofanyika kwa ajili ya matokeo fulani. Maamuzi ya leo ni hatma yako ya kesho.

Maamuzi yako ya leo yamebeba:

*Furaha yako ya kesho au huzuni.

*Heshima yako ya kesho au kudharaulika

*Nguvu zako za kesho.



Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/maamuzi-sahihi-katika-kuikabili-kesho-yako


Maamuzi sahihi ni yapi?

1.Kuamua mtu unayetaka kuwa kwenye maisha yako.

Watu wengi wanaishi huku wakiwa hawaelewi au hawajaamua nini hasa wanataka katika maisha yao. Walio wengi wanajaribu vitu vingi sana lakini hakuna kimoja au vichache ambavyo wanaamua kweli wanataka kuwa bora kwenye maisha yao.

Kumbuka kuwa mafanikio si matokeo ya kufanya vitu vingi bali ni matokeo ya kufanya kitu kimoja au vichache kwa mwendelezo.

Kumbe uamuzi wa kwanza na wa msingi ambao unapaswa kuufanya katika kuikabili kesho yako ni kuamua nini hasa unataka kuwa katika maisha yako.

Usisahau kuwa kila mwanadamu yupo duniani kwa kusudi maalumu, hakuna aliyekuja kuzurura.

Leo hii fanya uamuzi wa:

*Nini hasa unataka kuwa kwenye maisha yako.

*Maamuzi ya unataka dunia ikutambue kama nani

*Maamuzi ya kitu gani utajishughulisha nacho katika maisha yako


Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/1maamuzi


2.Kuwa tayari kulipa gharama ili kupata kile unachotaka.

Baada ya kuwa umefanya wa nini hasa unataka kuwa katika maisha yako, hatua ya pili na ya muhimu zaidi ni kufanya uamuzi wa kulipa gharama ili uweze kupata kile unachotaka kuwa katika maisha yako.

Kumbuka kuwa hakuna mafanikio yoyote yale yaliyopatikana bila kulipa gharama, ina maana kila kitu kwenye maisha kina gharama zake na utapata chochote kile kulingana na gharama unazolipa.




Zipo gharama za aina nyingi, Kwa mfano;

*Gharama ya muda

*Gharama ya kutafuta maarifa sahihi

*Gharama ya fedha

*Gharama ya kuachana na tabia fulani n.k


Ni muhimu ukatambua kuwa mafanikio makubwa yanahitaji gharama kubwa pia. Leo hii fanya maamuzi ya kulipa gharama stahiki kwa ajili ya aina ya mafanikio unayohitaji katika maisha yako huku ukitambua kuwa kiwango cha mafanikio utakayopata kinategemeana na aina na ukubwa wa gharama utakayolipa.

Je, leo hii unaamua kulipa gharama gani kwa ajili ya kesho yako?


Unaweza pia kusikiliza audio hii:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/2maamuzi


3.Kujikubali na kujitathmini.

Huu ni uamuzi wa msingi sana katika kuikabili kesho yako, haijalishi unapitia magumu au changamoto kiasi gani, uamuzi wa kujikubali ni wa msingi sana.

Watu waliofanikiwa wamekuwa watu wa kujikubali katika maisha yao. Unachopaswa kutambua ni kuwa changamoto zipo kukufanya imara na mwenye uwezo:kumbe basi magumu yasikufanye ukajidharau au ukajiona sio wa thamani.

Leo hii fanya uamuzi wa:

*Kujikubali

*Kujiona wa thamani

*Kujiona unastahili

*Kujiona unaweza.



Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/3maamuzi


4.Kusamehe na kujisamehe.

"Forgiveness doesn't change the past but enlarges the future"

Huu ni uamuzi wa msingi sana ambao unapaswa kuufanya katika maisha yako,kwa nyakati tofauti.Kumbuka kuwa tunasamehe kwa manufaa yetu wenyewe.

Inapokuja kwenye suala la mafanikio, amani ya moyo ni ya muhimu tena sana.Ni ajabu sana kuwasamehe wengine na wewe haujali msamaha mwenyewe katika makosa unayoyafanya ,kumbe pia wewe unastahili kujisamehe na kujifunza kutokana na makosa unayoyafaya.

Usisahau kuwa:

*Msamaha ni tiba ya roho .

*Tunasamehe kwa manufaa yetu wenyewe.

*Amani ya moyo ni kila kitu katika kuyatafuta mafanikio.

Amua kusamehe na kujisamehe.



Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/4maamuzi


5.Uamuzi  wa kutumia uwezo ulio ndani mwako.

Katika kuikabili kesho yako, huu ni uamuzi wa msingi ambao unapaswa kuufanya. Ni wazi na kweli kwamba kila mtu amezaliwa na uwezo wa kipekee (Uwezo unaotofautisha mtu mmoja na mtu mwingine)

Usipoweka juhudi katika kugundua kipaji chako ni vigumu sana kutimiza kusudi la kuumbwa kwako.

Njia za kugundua kipaji chako zipo nyingi ila za msingi unaweza:

*Kuangalia vitu unavyopenda zaidi katika maisha yako kumbuka hatupendi vitu bila sababu.

*Kuangalia eneo ulilobora zaidi.

Unaweza kuvipata hivi vyote kwa kusoma kitabu kiitwacho KIPAJI KILETACHO MAFANIKIO kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu UPENDO KITUNDU.


Unaweza pia kusiliza audio hii:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/5maamuzi



6.Uamuzi wa kuambatana na watu sahihi.

Watu unaoambatana nao wanaweza kuwa ngazi ya kukupandisha juu au wakawa watu wa kukuporomosha ushuke chini kabisa. Kuna watu waliokuwa na vipaji vikubwa sana ila kutokana na aina ya watu walioambatana nao ,hawajaweza kufika mbali.


Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/6maamuzi

7.Uamuzi wa kuwa na uhusiano na hatima yako.

Huu ni uamuzi wa msingi  tena sana ambao unapaswa kuufanya ili kuikabili kesho yako. Katika hili napenda kila mtu ajiulize swali hili, Nitakumbukwa kwa lipi duniani?

Je, unataka watu wakukumbuke kwa jambo gani ukiwa haupo tena duniani?

Mfano, Kama tunavyomkumbuka Mtume Paulo kama Nabii wa mataifa.



Unaweza kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/7maamuzi


Hitimisho:

Katika suala zima la kufanya maamuzi usisahau kuwa.

-Hakuna matokeo yoyote yale bila ya kufanya maamuzi.

-Unaweza kufanya chochote kile utakachoamua kufanya.

-Ni katika kufanya maamuzi ,hatima yako inapoundwa.

-Kutokufanya maamuzi ni maamuzi pia na yana matokeo yake.


Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/nini-cha-kujifunza-kwenye-kufanya-maamuzi

Comments

Popular posts from this blog

Mambo ya kuacha ili brand yako ifike mbali.

  Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/brand-utangulizi 1.Acha kuvaa brand za watu. Kuvaa brand za watu wengine badala ya kwako. Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/1brand 2. Kuwa adimu au usijirahisishe. Usijirahisishe waoneshe watu kuwa na maisha mazuri na unaweza kujitegemea bila watu. Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/2brand 3.Acha mazoea kwenye kazi. Usitoe huduma yako mahali kwa bure sababu ya mazoea. Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/3brand 4.Acha uongo na utapeli. Kuwa mwaminifu kwenye kazi yako,hio itakusaidia kutajwa mbele ya fursa. Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/4brand 5.Acha kujihurumia. Punguza kufatilia vitu visivyo na msingi na hakikisha unaongeza mda wa kazi yako. Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/5brand Kwa mahitaji bor...