Somo hili lilifundishwa na Juvenalis Makatu ambaye ni Raisi wa serikali ya wanafunzi chuo cha afya Musoma. Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/maamuzi Maamuzi ni azimio linalofanyika kwa ajili ya matokeo fulani. Maamuzi ya leo ni hatma yako ya kesho. Maamuzi yako ya leo yamebeba: *Furaha yako ya kesho au huzuni. *Heshima yako ya kesho au kudharaulika *Nguvu zako za kesho. Unaweza pia kusikiliza hii audio:https://audiomack.com/upendokitundu01/song/maamuzi-sahihi-katika-kuikabili-kesho-yako Maamuzi sahihi ni yapi? 1.Kuamua mtu unayetaka kuwa kwenye maisha yako. Watu wengi wanaishi huku wakiwa hawaelewi au hawajaamua nini hasa wanataka katika maisha yao. Walio wengi wanajaribu vitu vingi sana lakini hakuna kimoja au vichache ambavyo wanaamua kweli wanataka kuwa bora kwenye maisha yao. Kumbuka kuwa mafanikio si matokeo ya kufanya vitu vingi bali ni matokeo ya kufanya kitu kimoja au vichache kwa mwendelezo. Kumbe uamuzi wa kwanza na wa msingi amb...
Jukwaa maalumu la kimtandao linalojihusisha na uelimishaji wa jamii ya vijana.